Baadhi ya viongozi kutoka mrengo wa Kenya Kwanza kutoka kaunti ya Kisii wakiongozwa naye Kiranja wa Bunge la Kitaifa SYLVANUS Osoro wamekariri msimamo wao wa kutounga mkono aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani daktari Fred Matiangi akisema eneo hilo linasalia serikalini.
Wakizungumza katika kanisa la Matangamano kule Mugirango Kusini, viongozi hao waliirai jamii ya Abagusii kusalia pamoja na kutogawanywa na siasa za upinzani wakisema kamwe hawatatoka ndani ya serikali kuunga mkono Matiangi katika azma yake ya kuwania urais. Aidha katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa na msaidizi wa Rais, Farouk Kibet, alisisitiza kuwa siasa za migawanyiko kamwe hazitaruhusiwa nchini.