- 810 viewsDuration: 2:29Nao viongozi wa Kenya Kwanza waliendeleza shutuma zao dhidi ya muungano wa upinzani wakidai kuwa wanawapotosha wananchi badala ya kutafuta suluhu ya changamoto zinazoikabili nchi. Wakizungumza mjini Funyula, viongozi hao wamewataka Wakenya kuangazia miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali ya Kenya Kwanza na kupuuza ukosoaji kutoka kwa upinzani.