- 948 viewsDuration: 3:01Baadhi ya Viongozi wa Kenya Kwanza wamewasuta viongozi wa upinzani wakidai wanaeneza siasa za kuwagawanya wakenya kimaeneo na kikabila. Wakizungumza huko Shinyalu kaunti ya Kakamega, Cherangany katika Kaunti ya Trans Nzoia, na Funyula kaunti ya Busia, kibwagizo chao kilikuwa kusifia miradi ya maendeleo inayofanikishwa na utawala wa rais William Ruto, na kuitaka jamii ya mulembe kushikamana na kumpa rais ruto muhula wa pili kwenye uchaguzi wa mwaka ujao.