Skip to main content
Skip to main content

Viongozi wa upinzani wataka usalama wa Juni 25

  • | Citizen TV
    2,630 views
    Duration: 1:45
    Viongozi wa upinzani sasa wanataka waandamanaji kupewa uhuru na usalama wa kutosha wakati wa maadhimisho ya juni 25 ya kuwakumbuka vijana waliouawa wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha miaka miwili iliyopita. Wakizungumza katika hafla tofauti, viongozi hao wanashikilia kuwa waandamanaji wana haki ya kufanya maadhimisho kote nchini bila kutishiwa usalama wao kama vuiongozi wa serikali walivyotangaza katika siku za hivi punde. Akizungumza jijini Kisumu, gavana wa Siaya James Orengo amemkashifu rais William Ruto kwa kutoa amri ya kuthibiti waandamanaji huku naye naibu kinara wa Jubilee Fred Matiang'i aliyezungumza hapa Nairobi akizitaka asasi za usalama kutomdhuru yeyote atakayeshiriki maandamano siku ya Alhamisi.