Skip to main content
Skip to main content

Volkano iliyopeleka lava katika bahari ya hindi

  • | BBC Swahili
    32,581 views
    Duration: 52s
    Picha za angani zilizorekodiwa kwa kutumia droni zinaonesha lava ikitiririka kutoka kwenye volkano ambayo imekuwa ikilipuka kwa zaidi ya mwezi mmoja katika Kisiwa cha Réunion. Tarehe 15 Machi, lava kutoka volkano ya Piton de la Fournaise ilifika katika Bahari ya Hindi kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 19. Volkano hiyo ilianza kulipuka tarehe 13 Februari, ikiwa ni mara ya pili kufanya hivyo mwaka huu. Tangu wakati huo, mito miwili ya lava imesababisha uharibifu wa barabara kuu inayounganisha kusini na mashariki mwa kisiwa hicho. Mwandishi wa BBC Caro Robi na taarifa hii - - #bbcswahili #volkano #bahari #foryoü Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw