- 688 viewsDuration: 1:34Waathiriwa wa dhuluma katika kambi ya kijeshi ya British Army Training Unit Kenya wameendelea kushinikiza kupatiwa haki huku Kenya na United Kingdom zikitarajiwa kusaini mkataba mpya wa ushirikiano. Waathiriwa hao wameeleza kwa hisia namna walivyopitia changamoto na kuteseka kwa muda mrefu kutokana na madai ya dhuluma zinazohusishwa na wanajeshi wa Uingereza walioko kwenye kambi hiyo. Wanaharakati wa haki pamoja na familia za waathiriwa waliokutana mjini Nanyuki wamekosoa hali hiyo wakisema baadhi ya matukio yameathiri hata watoto waliozaliwa na kutelekezwa. Sasa wanataka suala la haki kwa waathiriwa lipewe kipaumbele hata wakati serikali ikijiandaa kusaini mkataba mpya wa ushirikiano na Uingereza.