Skip to main content
Skip to main content

Waathiriwa wa maandamano walalamikia kutengwa kwenye fidia

  • | Citizen TV
    750 views
    Duration: 3:30
    Baadhi ya waathiriwa wa maandamano ya mwaka 2024 na 2025 wamejitokeza kulalamikia kutengwa katika mchakato wa kufidiwa. Waathiriwa hao wanasema hawakuorodheshwa kupokea fidia licha ya kudhulumiwa na polisi. Baadhi yao, ambao ni miongoni mwa waliotekwa nyara, wanasema licha ya kujitokeza na kujisajili katika afisi za Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu, wameachwa nje ya orodha ya walionufaika bila kupewa sababu maalum.