- 225 viewsDuration: 3:15Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana katika makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha kujadili bajeti ya mwaka wa 2026/2027 ambayo makadirio yake ni dola million 110.8. Mkutano huu wa tatu, kikao cha nne cha Bunge la tano la kikanda, unatajwa kuwa na umuhimu mkubwa kiuchumi na kisheria kwa jumuiya, kwa sababu utatoa mwelekeo wa kibajeti na kifedha kwa mwaka ujao wa fedha.