- 633 viewsDuration: 3:39Siku mbili baada ya serikali kuongeza bei ya mafuta ya petroli na dizeli kwa shilingi 16 na 46 mtawalia, wachuuzi wa vyakula sasa wanaonya kuwa huenda bei ya vyakula ikaongezeka pakubwa katika siku zijazo. Kulingana nao, nyongeza ya bei ya mafuta itaathiri kwa kiasi kikubwa usafirishaji wa vyakula kutoka mashambani hadi mijini.