- 14,861 viewsDuration: 3:05Wakazi wa kijiji cha Furunzi huko Malindi, kaunti ya Kilifi wamesifia hukumu ya miaka 200 jela iliyotolewa dhidi ya mhubiri tata paul Mackenzie, wakishabikiashoka la jaji Diana Kavedza Mochache. Wakazi hao wametaja hukumu hiyo kama haki kwa familia na waathiriwa wa mauaji ya halaiki shakahola. Na kama anavyoarifu sasa Francis Mtalaki, kanisa aliloanzisha Mackenzie la Good News International kijijini humo sasa limesalia mahame.