- 7,550 viewsDuration: 3:13Ni mwaka wa 11 tangu kumwagika kwa mafuta kutoka kwenye mabomba ya Kenya Pipeline katika kijiji cha Thange, eneo la Kibwezi, Kaunti ya Makueni, na wakazi bado wanalalamikia athari za mafuta hayo. Wakazi hawa wamekuwa wakilalamikia matatizo mbalimbali ya kiafya ambayo sasa wanadai yanasababisha hata vifo. Michael Mutinda alizuru kijiji hiki na kutuandalia taarifa ifuatayo.