- 1,469 viewsDuration: 2:58Wakenya wamelazimika kulipa nauli za juu kufuatia kupanda kwa gharama ya mafuta ya petroli na dizeli. Vyama vinavyowakilisha sekta ya usafiri vimetangaza kupanda kwa nauli kwa asilimia 50. Aidha, vyama hivyo vimepanga mgomo wa kitaifa utakaojumuisha sekta ya matatu, bodaboda na teksi za kibinafsi kulalamikia gharama ya juu ya bidhaa hiyo.