- 1,295 viewsDuration: 2:45Huku saa zikiwa zimesalia saa chache kabla ya sherehe za krismasi, wakenya walioko vijini wamejiandaa vilivyo kwa sherehe hizo. Katika kaunti ya Vihiga, shamrasharma za sikukuu zimetanda kote huku familia nyingi zikitenga kuku na hata bata kama chakula spesheli cha krismasi, wakisema kuwa ni desturi kwao kula mapochopocho licha ya gharama ya maisha kupanda maradufu.