- 6,794 viewsDuration: 2:52Wakenya wawili ni miongoni mwa watu watano walioshtakiwa kwa wizi wa utambulisho katika sakata ya ulaghai wa ufadhili wa masomo nchini Marekani. Wakenya hao wanahusishwa na genge la matapeli linalodaiwa kusajili wanafunzi hewa katika vyuo vikuu vya Marekani na kuilaghai serikali ya nchi hiyo mabilioni ya shilingi kupitia ufadhili wa masomo. Sakata hiyo inakadiriwa kuigharimu serikali ya Marekani takriban shilingi bilioni 16.