- 384 viewsDuration: 3:06Idadi kubwa ya walimu nchini Kenya wamelalamikia ongezeko la ushuru kwa Mishahara yao bila maelezo mwafaka kutoka kwa Tume ya Kuajiri walimu TSC. Katika mishahara yao ya mwezi Juni, baadhi ya walimu waligundua makato ya hadi shilingi 108 ambayo inafikia jumla ya hadi shilingi milioni 32.4 iwapo itakatwa kwa Mwalimu wote 300,000 ambao wameajiriwa na tume hiyo. Naibu katibu mkuu wa KNUT Hesborne Otieno ameitaka TSC kuweka bayana kilichosababisha makato hayo