Walimu wakimbizi katika kambi ya Kakuma, kaunti ya Turkana, wamekuwa wakifundisha kwa miaka mingi bila kutambuliwa na mfumo rasmi wa Serikali ya Kenya.
Baadhi yao wamezaliwa na kusomea nchini Kenya lakini wanakabiliwa na changamoto ya kukosa vitambulisho, hali inayowazuia kuingia katika mfumo rasmi wa uajiri wa walimu.
Walimu hao, ambao kwa sasa wanategemea mishahara kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali, wamesema wanapitia changamoto kubwa za maisha kutokana na hali hiyo. Emily Chebet anaripoti zaidi kuhusu hali yao.