- 2,274 viewsDuration: 2:57Walimu wa shule za upili sasa wanapendekeza wanafunzi watukutu wanaojihusisha na migomo na uharibifu wa mali kupigwa marufuku kushiriki mitihani ya kitaifa. Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wakuu nchini Willie Mwangi Kuria pia akitaka Baraza la Mitihani nchini kuwaondoa kwenye sajili wanafunzi hao akisema baadhi yao hubadilika baada ya kusajiliwa. Walimu wakuu pia wanapendekeza kubadilishwa kwa tarehe ya kusajiliwa kwa watahiniwa.