Skip to main content
Skip to main content

Wapigaji makasia 50 waingia kikosi cha Taifa kuelekea Kombe la Dunia

  • | Citizen TV
    382 views
    Duration: 1:43
    Jumla ya wapigaji makasia 50 wameteuliwa kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Kenya kinachojiandaa kwa michuano ya Kombe la Dunia ya upigaji makasia itakayofanyika nchini mwezi Julai. Katika mchujo wa kitaifa wa siku mbili uliowashirikisha zaidi ya wanariadha 120, wachezaji hao 50 wamefanikiwa kupata nafasi baada ya ushindani mkali wa kuwania tiketi ya kuwakilisha nchi. Kenya itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo kuanzia Julai 6 katika eneo la Sagana, ikiwa ni mara ya kwanza kwa taifa la Afrika kuandaa mashindano hayo. Tayari mataifa 19 yamekamilisha uthibitisho wa kushiriki katika michuano hiyo ya wiki moja.