Watu sita wamefariki huku wengine kadhaa wakijeruhiwa kufuatia shambulizi dhidi ya gari la abiria katika kaunti ndogo ya Arabia, kaunti ya Mandera.Shambulizi hilo lilitokea katika mtaa wa Ber Cawayon eneo la Harer leo majira ya adhuhuri, ambapo watu wenye silaha walilishambulia gari lililokuwa likielekea katika mji wa Arabia. Tukio hilo limeibua tena wasiwasi kuhusu hali ya usalama katika eneo hilo.Asasi za kiusalama zimeanzisha oparesheni ya kuwasaka wahusika wa shambulizi hilo. Mamlaka husika zimesema uchunguzi bado unaendelea huku majina ya waathiriwa yakisubiri kutolewa rasmi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive