- 259 viewsDuration: 1:10Watu wenye ulemavu wamehimizwa kujitokeza kuwania nyadhifa za kisiasa ili waweze kuwakilisha maslahi yao moja kwa moja katika ngazi mbalimbali za uongozi. Wadau wanasema ushiriki wao katika siasa utasaidia kuhakikisha sauti na mahitaji ya watu wenye ulemavu yanazingatiwa katika utoaji wa huduma na utungaji wa sera.