- 1,230 viewsDuration: 3:07Wazazi wa wanafunzi ishirini na mmoja waliofariki Kwenye mkasa wa moto shuleni Hillside Endarasha miaka miwili iliyopita, wanasema serikali imewatelekeza licha ya ahadi kuwa wangepata msaada wa kutosha hadi watakapopata haki. Wakizungumza mjini Nyeri, Wazazi hao walioeleza Uchungu wanaoendelea Kupitia kwenye safari ya kutafuta ukweli wa matukio ya Septemba tano mwaka 2024, pia wamemnyoshea kidole cha lawama Mkurugenzi wa mashataka ya umma kwa kuchelewesha uchunguzi unaoendeshwa na mahakama ya Nyeri.