- 1,280 viewsDuration: 1:21Imebainika kuwa baadhi ya wazee wa mitaa kutoka kaunti ya Bungoma hawajapokea malipo yao ya kila mwezi, licha ya serikali kutangaza kuwa mpango huo unalenga kuwafidia wazee wanaohudumu katika jamii. Baadhi ya wazee hao kutoka Kata ya Sirende, Webuye Magharibi, wanasema majina yao hayakuorodheshwa kwenye sajili iliyowasilishwa na machifu wao, hali ambayo imewafanya kukosa malipo yao.