- 3,680 viewsDuration: 2:37Wakazi wa Kisumu wanalalamikia ongezeko la visa vya wizi wa kimabavu. Katika wiki moja iliyopita, mtu mmoja ameuawa, makumi ya wengine kujeruhiwa na maduka kuvunjwa na magenge ya wezi waliojihami. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, Kamishna wa Kaunti ya Kisumu, Ramadhan Mwadubzo, amesema kuwa msako utaanza wiki ijayo na kuwataka wakazi kushirikiana na polisi ili kuwanasa wahalifu hao.