Skip to main content
Skip to main content

Zaidi ya familia 10 zakadiria hasara ya moto wa usiku eneo la Litein, Kericho

  • | Citizen TV
    236 views
    Duration: 1:56
    Familia zaidi ya kumi huko Litein katika eneobunge la Bureti wanakadiria hasara kubwa baada ya nyumba zao kuteketezwa na moto usiku wa kuamkia leo. Kulingana na walioshuhudia tukio hilo, moto ulizuka wakati wa usiku wakazi walipokuwa wamelala. Mama mmoja anauguza majeraha katika hospitali ya misheni ya AIC Litein. Wakazi wa eneo hilo wamewashutumu zimamoto wa kaunti wakisema walichelewa kufika kuuzima moto huo. Wakizungumza baada ya mkasa huo, wakazi, wameipa serikali ya kaunti makataa ya wiki moja kuhakikisha magari ya zimamoto yanarejeshwa katika kituo kikuu cha Bureti ili kusaidia kukabiliana na dharura siku zijazo.