- 103 viewsMaelfu ya watu wamekusanyika katika miji mbalimbali kote Ugiriki Ijumaa kushinikiza haki ifanyike katika maadhimisho ya pili ya ajali mbaya ya treni kuwahi kutokea, huku wafanyakazi katika sekta ya usafiri wa ndege, majini na treni wakigoma. Watu 57 walifariki wakati treni ya abiria iliyokuwa imejaa wanafunzi ilipogongana na treni ya mizigo Februari 28, 2023, karibu na Tempi gorge huko katikati ya Ugiriki Miaka miwili baadaye, mianya ya usalama ambayo ilisababisha ajali hiyo haijatatuliwa, uchunguzi ulionyesha hivyo Alhamisi. Uchunguzi wa kujitegemea wa mahakama bado haujakamilika, na hakuna aliyehukumiwa katika ajali hiyo. Maandamano ya umma yalikuwa yamepangwa kufanyika katika darzeni ya miji kote nchini. Safari zote za ndege za ndani na za kimataifa zilisitishwa wakati waongoza ndege wakiungana na waendesha feri, treni, madaktari, mawakili na waalimu katika mgomo wa jumla wa saa 24 kuwaenzi waathirika wa ajali hiyo. Biashara zilifungwa na majumba ya burudani yalifuta maonyesho. Hadi kufikia asubuhi, maelfu walikuwa wamekusanyika katika Bustani ya Syntagma katikati ya Athens, huku wakisimamiwa na askari wa kuzuia ghasia. Bango moja lilisoma: “Serikali ni wauaji.” Serikali ya mrengo wa kati-kulia ya Waziri Mkuu Kyriakos Mitsotakis ambayo ilishinda tena uchaguzi baada ya ajali ya mwaka 2023, imekabiliwa na ukosoaji mara tena kutoka kwa ndugu wa wahanga kwa kushindwa kuanzisha uchunguzi wa bunge ikiwa ni kuwajibika kisiasa. Serikali imekanusha kufanya makosa yoyote na kusema ni juu ya mahakama kuchunguza ajali hiyo. - Reuters #athens #ugiriki #ajali #treni #mahakama #mgomo #wafanyakazi #ndege #majini #treni
Maelfu ya watu wakusanyika miji mbalimbali kushinikiza haki ifanyike
- - Duniani Leo ››
- - Local news roundup ››
- 16 Jun 2025 - Residents of Elgeyo Marakwet County are raising alarm over a growing shortage of condoms, a situation that has been blamed for a spike in new HIV infections. According to Professor Sylvester Kimaiyo, Chief of Party at the Academic Model Providing Access…
- 16 Jun 2025 - Rescue operations are ongoing in the Kambi Karaya area of West Pokot County following the collapse of a gold mine. According to police reports, one body has been recovered, while several others remain unaccounted for. The incident was reported at Marich…
- 16 Jun 2025 - Official says Iran appealed to Oman and Qatar to engage the US to broker a ceasefire.
- 16 Jun 2025 - The Iranian death toll in four days of Israeli strikes had reached at least 224, with 90 per cent of the casualties reported to be civilians.
- 16 Jun 2025 - Assassination of Kasipul MP Ong’ondo Were, death of teacher Albert Ojwang’ and ODM’s internal rebellion have shaken the foundation of Ruto-Raila pact.
- 16 Jun 2025 - More than 100,000 small businesses across the country will benefit from a KSh5 billion grant to boost the enterprises, President William Ruto has announced. The President said the government, in partnership with the World Bank, will provide KSh50,000 to…
- 16 Jun 2025 - Hidden knife in the Finance Bill that stabs firms
- 16 Jun 2025 - Security budget balloons while justice starves and protesters bleed
- 16 Jun 2025 - Police explanation of Ojwang's death comes from a familiar past script
- 16 Jun 2025 - Cancer took my health, heartbreak everything else: Leah Wanjiru's silent battle