Bunge la seneti kusikiliza pendekezo la kubanduliwa kwa gavana wa Isiolo

  • | KBC Video
    88 views

    Pendekezo la kumwondoa mamlakani gavana wa Isiolo Abdi Guyo litasikizwa na bunge nzima la seneti baada ya seneti kukosa kuidhinisha hoja ya kubuni kamati maalum ya kuchunguza madai dhidi ya gavana huyo. Hoja hiyo iliyowasilishwa na seneta wa Kakamega Bonny Khalwale kwa niaba ya kiongozi wa wengi katika bunge la seneti, ilipendekeza kubuniwa kwa kamati ya wanachama 11 kuchunguza madai hayo. Hata hivyo, pendekezo hilo halikufanikiwa baada ya seneta wa Kilifi Stewart Madzayo, aliyetarajiwa kuunga mkono hoja hiyo, alipoipinga, hivyo kumlazimu spika Amason Kingi kuagiza kwamba suala hilo liangaziwe na bunge nzima.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive