Vipande vya ardhi kulipia deni linalodaiwa KBC na waliostaafu

  • | KBC Video
    107 views

    Mpango wa malipo ya kustaafu wa shirika la utangazaji humu nchini, KBC umetoa wito kwa bunge kuiomba ofisi ya Rais kuidhinisha pendekezo la kugawiwa baadhi ya vipande vyake vya ardhi ili kulipia deni la shillingi billioni 3.2 ambazo wafanyakazi wa KBC waliostaafu wanalidai shirikahilo kama matozo ya kila mwezi ambayo hayakuwasilishwa.Wadhamini wa mpango huo waliofika mbele ya kamati yabunge la kitaifa kuhusu habari na teknolojia ya mawasiliano , walisema bodi ya wasimamizi ya KBC imeidhinisha uhamishaji wa vipande hivyo vya ardhi na sasa suala hilo liko mbele ya wizara ya habari na utangazaji. Wadhamini hao pia walitoa wito kwa wabunge kuchunguza jinsi wadhamini wa zamani walivyotoa kwa njia isiyo halali zabuni ya huduma za kisheria ambazo zingeugharimu mpango huo zaidi ya shillingi billioni 1.4.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive