Skip to main content
Skip to main content

Wakazi waonywa dhidi ya biashara haramu ya pombe katika Kaunti ya Nandi

  • | Citizen TV
    295 views
    Duration: 1:12
    Wakazi katika Kaunti ya Nandi wametakiwa kupata leseni ya kuandaa pombe ya kienyeji ya busaa, ili kuzuia biashara ya pombe haramu wakati wa sherehe za kitamaduni. Akizungumza mjini Kapsabet wakati wa hafla ya kuzindua wiki ya uhamasishaji ya NACADA, Naibu Kamishna Nandi ya Kati Alfet Jillo amesema ni muhimu kutenganisha tamaduni na shughuli zinazokiuka sheria kwa kisingizio cha utamaduni. Jillo, amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuhusika na shughuli za kitamaduni ili kutengeneza na kuuza pombe haramu kinyume na sheria.