- 1,548 viewsDuration: 3:08Zoezi la usajili wa makurutu lilikamilika kwa masikitiko kwa wale ambao hawakutimiza viwango vilivyotakiwa. Katika kaunti ya baringo, idris kiprop ni miongoni mwa walioambulia patupu na alikosa kufuzu kwa mwaka wa nane mfululizo. Kila mwaka idris amekuwa akifika akiwa na matumaini ya kusajiliwa katika idara ya polisi. Hata hivyo, kila mara kimo chake kimemnyima nafasi ya kuvalia sare anayotamani.