- 1,507 viewsDuration: 3:02Familia moja huko Makueni imejipata kwenye tanzia baada ya watu wanne kufariki kwa pamoja kwenye ajali ya barabarani huko Ngoluni kaunti ya Makueni. Wanne hao walikuwa mama na wanawe watatu waliokuwa wamesafiri kwenda kumchukua kijana wao ambaye alikuwa amekamilisha mtihani wa KCSE. Watoto wawili wa familia hiyo wanapokea matibabu baada ya kunusurika kifo. Ajali hiyo iliyotokea katika barabara ya Itangini kuelekea Tawa huko Mbooni mashariki iliwauwa watu sita.