- 511 viewsDuration: 2:22Maandalizi ya awamu ya tatu ya mbio za nyika za Chepsaita yanaendelea vyema. Mfadhili wa mbio hizo Farouk Kibet amekagua uwanja wa Chepsaita, akieleza kwamba kila kitu kitakuwa tayari kwa wakati. Kibet, alitembelea uwanja huo pamoja na maafisa wa shirikisho la riadha nchini AK na wanachama wa kamati ya kuandaa shindano hilo.