Skip to main content
Skip to main content

Viongozi wa serikali ya Embu watoa madai ya vurugu kutoka upinzani kwenye uchaguzi mdogo kesho

  • | Citizen TV
    2,207 views
    Duration: 3:17
    Katika eneo bunge la Mbeere North, viongozi wanaoegemea upande wa serikali kaunti ya Embu wakiongozwa na mwenyekiti wa UDA Cecily Mbarire wamedai kuwa viongozi wa upinzani wanapanga kuzua vurugu hapo kesho. Madai haya yakijiri huku usalama ukiimarishwa na maafisa wa polisi wakiweka vizuizi katika barabara zote kuu za kuingia na kutoka Embu. Vifaa vya kupigia kura vimesambazwa vituoni, tayari kwa uchaguzi ambapo wagombea 9 wanatarajiwa kukabana koo.