- 648 viewsDuration: 2:01Kikundi cha Waangalizi wa Uchaguzi (ELOG) kinasema IEBC ilifanya vizuri katika uchaguzi mdogo uliokamilika licha ya fujo zilizoripotiwa katika maeneo kadhaa pamoja na changamoto za mitambo ya kielektroniki. Hata hivyo, ELOG imeitaka tume hiyo na polisi kuchukua hatua pale ambapo ukiukaji wa sheria za uchaguzi umefanyika, kuongeza elimu ya wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027 na pia kuhakikisha kwamba vyama vya siasa na wagombea wameacha kuingilia mchakato wa uchaguzi.