- 738 viewsDuration: 1:30Chama cha Walimu wa Shule za sekondari msingi, KEJUSTA, kimejitokeza tena kutaka uhuru kamili wa Shule hizo, kikisema wanafunzi na walimu wa JSS wana mahitaji ya kipekee yanayohitaji uongozi maalum. Katika taarifa yao, chama hicho kimezitaka KUPPET, TSC, Wizara ya Elimu na Rais kushirikiana na walimu wa JSS huku kikisema utekelezaji wa mtaala wa CBE una mapungufu ya kimfumo na kiutawala.