- 428 viewsDuration: 2:50Wakazi wa maeneo ya Kima, kawese na mangala katika eneo la Kilome kaunti ya Makueni wameitaka serikali ya kaunti hiyo kukabiliana na watu wanaozoa mchanga kinyume cha sheria za kaunti hiyo na kuendelea kuharibu mazingira. Wakazi hao sasa wanasema shughuli hiyo imesababisha mito kukauka na kuwalazimu kwenda mbali kutafuta maji.