- 11,713 viewsDuration: 1:58Wabunge nchini Bulgaria wamekubaliana bila kupinga - uamuzi wa baraza la mawaziri kujiuzulu madarakani, siku moja baada ya kukabiliwa na shinikizo kubwa nchini kwa madai ya kushiriki ufisadi. Hatua hii inafanyika siku chache tu baada ya dunia kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupambana na ufisadi. Waziri Mkuu wa nchi hiyo na serikali yake, walitangaza kwamba wangeondoka madarakani, kabla hata ya kumaliza mwaka mmoja uongozini. Hii ni kutokana na maandamano ya kuupinga uongozi huo, tuhuma za ufisadi kukithiri serikalini na bajeti ya kitaifa iliyosemekana kuwa na utata mkubwa. Kuanguka kwa serikali hii kunafungua upya mlango mwingine wa mazungumzo ya kubuni serikali ya muungano, kupitia kile ambacho wachambuzi wengi wa kisiasa wanasema ni uchaguzi mpya. - - #bbcswahili #Uongozi #ufisadi #bulgaria Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw