- 347 viewsDuration: 1:28Wakazi katika eneo mbunge la Ndaragwa Kaunti ya Nyandarua wametaka polisi watumie mbwa wa kunusa kuwanasa wezi wa mifugo ambao wamekuwa wakiwahangaisha eneo hilo. Wamedai kuwa visa vya wizi wa mifugo, uvunjaji wa nyumba na maduka vimekuwa vikiongezeka kila kuchao lakini hakuna mshukiwa yeyote ametiwa baroni. Kulingana na wakazi, wahalifu hao huwaibia na kutorokea katika Msitu wa Ndaragwa.