- 4,479 viewsDuration: 2:52Baraza la mawaziri leo limeidhinisha kubuniwa kwa hazina ya kitaifa ya miundo msingi na hazina ya kitaifa ya utajiri wa nchi, kusaidia kuanzisha safari ya kubadilisha kenya kuwa mojawapo ya mataifa tajiri zaidi duniani. Kupitia kwa taarifa kutoka ikulu ya rais, baraza la mawaziri pia limeratibu kuwa hazina ya miundo msingi itabuniwa kama kampuni binafsi itakayosaidia kuboresha barabara, mabwawa na miundo msingi nchini