Skip to main content
Skip to main content

Watu wawili wateketea hadi kufa kijijini Makunga, Kitale

  • | Citizen TV
    5,186 views
    Duration: 1:58
    Watu wawili wamefariki baada ya kuteketezwa na moto uliozuka usiku wa kuamkia leo katika eneo la Makunga, viungani mwa mji wa Kitale. Majirani wanasema chanzo cha moto huo hakijabainika. Moto huo ulioanza mwendo wa saa tisa usiku uliangamiza mwanamke mmoja pamoja na mmiliki wa ploti hiyo. Polisi wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo.