- 493 viewsDuration: 38sOmbi limewasilishwa katika Mahakama ya Milimani likitaka IEBC izuiwe kuendesha uchaguzi wowote hadi ikamilishe mapitio ya kikatiba ya mipaka ya maeneo ya uchaguzi na wadi. Mlalamishi Philip Kipkemoi Langat anasema mapitio ya mwisho yalifanyika mwaka 2012, kinyume na Ibara ya 89 inayotaka mapya yakamilike Machi 2024. Anadai IEBC haijaanzisha zoezi hilo licha ya kutangazwa Julai 2025, huku uchaguzi mdogo wa Isiolo Kusini ukipangwa Februari 26 mwakani.