Wanafunzi ambao wangali wanatafuta usaidizi kuhusiana na suala la kujiunga na gredi ya 10 wana fursa nyingine ya kutuma barua za kurejelewa kwa maombi yao baina ya tarehe 6 na 9 mwezi Januari mwaka 2026. Kwa mujibu wa waziri wa elimu Julius Migos, maombi yaliyokosa kuidhinishwa yalihusishwa pakubwa na kutojumuishwa kwa masomo hitajika au kutokuwa na uwezo wa kuwapokea wanafunzi katika shule walizochagua. Wizara ya elimu ilipokea malalamishi 355,457 ili kuyarejelea huku kila mwanafunzi akiruhusiwa kutuma maombi manne. Jumla ya wanafunzi 211, 636 walipokea idhinisho ya kurejelewa kwa maombi yao.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive