- 22,908 viewsDuration: 1:21“…Unajua magumu yaliyokupata wewe, yalikupata kwa sababu mimi nilikataa utekaji. Mpaka leo nakataa vilele…,” Kiongozi wa makanisa ya Ufufuo na Uzima Askofu Josephat Gwajima ameibuka kanisani kwake katika mkesha wa mwaka mpya na kuwaeleza wafuasi wake kuwa angali anapinga vitendo vya utekaji nchini Tanzania. Gwajima alitoa mahubiri kwa mara ya mwisho atika kanisa hilo lililopo Ubungo jijini Dar Es Salaam mwezi Juni 2025 kabla ya kanisa hilo kufungiwa na kuzingirwa na polisi. Kanisa hilo lilifunguliwa mwishoni mwa Novemba mwaka jana kwa maelekezo ya Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba. Gwajima ambaye alikuwa mbunge wa chama tawala nchini Tanzania alijitokeza katikati ya mwaka 2025 kuwa mpaza sauti dhidi ya matukio ya utekaji ya watu hususan walioonekana kuwa wakosoaji wa serikali. Serikali imekuwa ikijitenga na matukio hayo ya utekaji lakini ingali inanyooshewa kidole cha lawama. - - #bbcswahili #gwajima #siasa #dini #utekaji Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw