Rais William Ruto atoa hakikisho kuhusu kawi safi

  • | Citizen TV
    849 views

    Rais William Ruto ametoa hakikisho kwamba kenya itaendelea kufanya kipaumbele juhudi za kuhakikisha utumizi wa kawi safi barani Afrika. Kwenye mazungumzo na rais wa kongamano la kimataifa la 26 kuhusu mabadiliko ya tabianchi, alok sharma katika ikulu ya Nairobi, Rais Ruto amesema kuwa Kenya itahakikisha imeweka mikakati ya kudhibiti mabadiliko hayo. Aidha Rais Ruto amesema mabadiliko ya tabianchi ni tisho kubwa kwa afya ya umma, ajira na utoshelevu wa chakula.