Kundi la wanasiasa wanaoshughulikia haki za watoto wa kiume katika kaunti ya Embu limetaka kuangaliwa upya kwa sheria za dhulma za kingono nchini Kenya, wakisema baadhi ya vifungu vinahusisha adhabu kali na kulenga vijana wa kiume kwa njia isiyofaa. Shirika la kutetea haki za mtoto wa kiume kwa jina Boy Child justice Alliance linasema kuwa hukumu za lazima chini ya sheria za ubakaji huhusisha kifungo cha muda mrefu, kikizuia nafasi za kurekebisha tabia, hasa katika kesi zinazohusisha uhusiano wa kimapenzi miongoni mwa vijana.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive