- 528 viewsDuration: 1:22Naibu kinara wa ODM Abdulswamad Shariff Nasir anasema mazungumzo kati ya ODM na UDA ni kwa minajili ya kuhakikisha chama cha chungwa kinawasilisha matakwa yatakayonufaisha wanachama na uungwaji mkono wa chama hicho nchini. Akizungumza huko Mombasa gavana huyo wa Mombasa amewataka wanaopinga hoja hiyo kusubiri hadi pale viongozi wa vyama hivyo watafanya kikao na kuweka bayana maelewano badala ya kupinga ushirikiano wa UDA na chama cha chungwa.