Skip to main content
Skip to main content

Mbunge Caleb Amisi adai chama cha ODM kinayumbishwa na serikali

  • | Citizen TV
    415 views
    Duration: 1:13
    Mbunge wa Saboti Caleb Amisi amedai kuwa chama cha ODM kimeuzwa kwa serikali, akisema baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho wanatengwa na uongozi wa sasa. Akizungumza huko Trans Nzoia, wakati wa hafla ya kutoa fedha za ufadhili kwa wanafunzi, Amisi amesema tangu aliyekuwa kinara wa chama Raila Odinga kuaga dunia, ODM imekumbwa na migawanyiko mikubwa. Amisi akidai serikali inahusika na migawanyiko hiyo.Aidha ameonya kuwa iwapo baadhi ya viongozi wataendelea kutengwa, yeye na wenzake wanaweza kujiondoa ODM na kuanzisha chama kipya kabla ya uchaguzi mkuu ujao.