- 14,291 viewsDuration: 46sNi mwaka mmoja sasa tangu Donald Trump kuapishwa kama Rais wa Marekani kwa awamu ya pili. Na katika miezi 12 iliyopita, ametenda mengi katika kutekeleza ajenda yake ya 'MAKE AMERICA GREAT AGAIN' na 'AMERICA FIRST'. Trump ambaye amekuwa akifuatilia sana tuzo ya amani ya Nobel, anasema kwamba hana hamu tena ya kutafuta amani duniani baada ya kuingilia vita kati ya mataifa kadhaa kwenye mabara yote. Azimio lake ni kuilinda Marekani na hatosita kuchukuwa hatua za kijeshi kama alivyofanya nchini Venezuela kuhakikisha hilo limefanyika. Mwaka wa kwanza madarakani unapokamilika, dunia itarajie nini kipya kutoka kwa Trump? @HamidaAbubakar anachambua suala hili kwa kina saa tatu usiku kwenye Dira ya Dunia TV kwenye ukurasa wa YouTube wa BBC Swahili. #bbcswahili #marekani #DonaldTrump Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw