Kama njia ya kuhakikisha swara aina ya mountain bongo anaendelea kuongezeka kwa idadi baada ya kuwa kwenye hatari ya kuangamia, wadau wanaoshiriki uhifadhi wa wanyamapori, wamezindua mpango wa Centinella, ambao unazishirikisha satelaiti kuwafuatilia Wanyama hao kwa nia ya kubaini mazingira bora zaidi ya swara hao kuzaana.
Mpango huo unaoendeshwa na shirika la anga ya Kenya, utashirikishwa kutambua mazingira ndani ya misitu ya Kakamega, Aberdare na mlima kenya wanakostawi, na pia kubaini wanavyoadhiriwa swara hao na mabadiliko ya tabianchi. Wakizungumza walipozindua utumizi wa mradi huo, wahifadhi hao wamezirai hifadhi zingine kukumbatia matumizi ya teknoloJia za kisasa, kuboresha juhudi za uhifadhi wa Wanyama pori.