Kenya na Marekani zimeafikiana kukuza ushirikiano katika masuala ya ulinzi, udumishaji amani na usalama. Hatua hii inanuiwa kuimarisha uthabiti wa kikanda pamoja na kusaidia katika ukuaji wa uchumi. Makubaliano hayo yalitangazwa wakati wa ziara ya naibu waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani Christopher Landau jijini Nairobi, ambapo alifanya mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu serikalini, akiwemo waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi. Awali, Landau alikutana na rais William Ruto katika ikulu ya Nairobi kukadiria uhusiano baina ya nchi hizo mbili na kujadili mbinu za kuimarisha ushirikiano wa siku za usoni.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive