Skip to main content
Skip to main content

Serikali kuongeza ufadhili wa matibabu ya saratani kupitia mfumo wa SHA

  • | KBC Video
    119 views
    Duration: 2:14
    Waziri wa afya Aden Duale amekariri uwajibikaji wa serikali katika kuimarisha upatikanaji wa matibabu ya saratani kupitia nyongeza ya fedha za matibabu ya ugonjwa huo chini ya hazina ya bima ya afya ya jamii kutoka shilingi laki tano hadi shilingi laki nane. Akizungumza katika hospitali ya matibabu maalum ya kaunti ya Mombasa alipokagua kituo kipya cha matibabu ya saratani, Duale alisema serikali itatenga fedha za kuhakikisha mashine zinazotumika katika matibabu ya ugonjwa wa saratani zinakarabatiwa. Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Nassir alitoa kipande cha ardhi kwa ujenzi wa wodi ya wagonjwa wa saratani katika hospitali hiyo. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive